JINSI YA KUTENGENEZA SUBTITLE AMBAYO UNAWEZA KUWEKA NA KUITOA KWENYE VIDEO
Kwa wale wanaopenda kujua mengi kuhusiana na teknolojia sasa na hii inakuhusu,tambua njia rahisi itakayoweza kukusaidia katika utengenezaji wa subtitle ambayo unaweza kuiweka ama kuitoa kwenye video yeyote.
kuna faida nyingi kama utaijua taaluma hii kama vile itakusaidia kupata pesa kama utaitumia vizuri pia inasaidia kukuza lugha kama vile lugha yetu ya kiswahili,hivyo basi tumia muda wako kidogo kufatilia maelezo haya,
kuna njia nyingi za kutengeneza subtitle kama kutumia progam specific kwa kutengeneza subtitle kama vile
AEGISUB ila mimi naelezea kwa NOTEPAD
MAHITAJI
komputa yeyote ya windows
USHAURI
ilikuelewa vizuri na kupata maelezo mazuri nakusihi angalia video fupi ya kiswahili kwenye link hapo chini inayoelezea maelezo haya
TUANZE
Fungua program ya notepad ambayo inapatikana kwenye computa yeyote ya windows,unaipata kwa kubofya sortcut ya windows na batani ya R (WIN + R),itafunguka run basi search notepad kwenye search box inayopatikana kwenye hiyo run
Ukishafungua angalia kanuni hii namba ya subtitle muda wa subtitle kuanza --> muda wa subtitle kuisha maneno yanayopatikana kwenye video kwa muda husika.
nikiwa ninamaamisha
namba 1 na kuendelea
muda unakua hivi
00:00:00,000 yaani saa:dakika:sukunde,minisekunde
kwahiyo inakuwa hivi
1
00:00:01:976 --> 00:00:04:186
jana usiku ulikuwa wapi?
2
00:00:05:123 --> 00:00:06:678
nakuuliza wewe mwanamke,mbona haujibu?
JINSI YA KUSAVE
Nenda juu ya notepad kushoto palikoandikwa file --> save as --- file name andika chochote kisha malizia na .srt
kwa mfano
ramar.srt na kwenye save as type weka all kisha save.
ramar.srt na kwenye save as type weka all kisha save.
Kama umeipenda hii basi like na share na wana kama kuna mahali haujaewa usikose kucomment
Kwenye hadroid haiwezekani
ReplyDelete